Submitted by kipala on 12 November 2008 - 11:24am.
Nimekuta maneno matatu yakitumiwa kwenye kamusi: kibonzo-katuni halafu mtandaoni: komiki.
Sasa kwa Kiingereza watu hutofautisha "cartoon" - ambayo ni picha moja na "comics/ comic strip" ambayo ni hadithi inayosimuliwa kwa picha mfululizo (yaani zaidi ya moja).
Sasa sina uhakika kama "kibonzo" kinaunganisha pande zote mbili au ni zaidi "cartoon". Vilevile sina uhakika kama "katuni" ni sawa na Kiing. "cartoon" au inajumlisha pia maana ya "comics".
Kibonzo kwa kawaida ni picha moja au mfuatano wa picha unaochekesha au kudhihaki.
"Comic" ni "gazeti" fupi lenye mtiriiko wa picha unaosimulia hadithi inayoburudisha kwa kiasi kikubwa.
Kwangu, "kibonzo" huegemea upande wa "cartoon" zaidi kuliki ule wa "comic".
"Comic" na "hadithi" ni vigumu kuzitenganisha.
"Kibonzo" na "comic" ni rahisi kuzitenganisha.
Kinadharia, "comic" inawezekana kutengenezwa kwa kutumia "vibonzo" (na kinyume chake). Lakini "akina yahe" haitumii maneno hayo mawili kama visawe.
Submitted by Chumvi Mtembezi on 14 November 2008 - 5:45am.
Kwenye Redio Tumaini mahali niliposikia kwa mara ya kwanza miaka si mingi sana iliyopita mbadala wa 'katuni', huwa wanatumia neno 'kiponzo'.
Nadhani 'kiponzo' au 'kibonzo' ni jitihada za kuongeza misamiati, badala ya 'kuhalalisha' matumizi ya 'katuni', neno ambalo lilikuwa linatumika toka enzi za utoto wetu.
Kibonzo ni sawa na katuni.
Kibonzo ni sawa na katuni. Yaani picha ya (za) kuleta ujumbe kwa njia ya kuchekesha.
Katuni
Katuni = Cartoon
Nimekuta maneno matatu
Nimekuta maneno matatu yakitumiwa kwenye kamusi: kibonzo-katuni halafu mtandaoni: komiki.
Sasa kwa Kiingereza watu hutofautisha "cartoon" - ambayo ni picha moja na "comics/ comic strip" ambayo ni hadithi inayosimuliwa kwa picha mfululizo (yaani zaidi ya moja).
Sasa sina uhakika kama "kibonzo" kinaunganisha pande zote mbili au ni zaidi "cartoon". Vilevile sina uhakika kama "katuni" ni sawa na Kiing. "cartoon" au inajumlisha pia maana ya "comics".
Je nani anaweza kusaidia?
Kibonzo
Haya maoni yangu machache, wanaukumbi:
Kibonzo kwa kawaida ni picha moja au mfuatano wa picha unaochekesha au kudhihaki.
"Comic" ni "gazeti" fupi lenye mtiriiko wa picha unaosimulia hadithi inayoburudisha kwa kiasi kikubwa.
Kwangu, "kibonzo" huegemea upande wa "cartoon" zaidi kuliki ule wa "comic".
"Comic" na "hadithi" ni vigumu kuzitenganisha.
"Kibonzo" na "comic" ni rahisi kuzitenganisha.
Kinadharia, "comic" inawezekana kutengenezwa kwa kutumia "vibonzo" (na kinyume chake). Lakini "akina yahe" haitumii maneno hayo mawili kama visawe.
Kiponzo
Kwenye Redio Tumaini mahali niliposikia kwa mara ya kwanza miaka si mingi sana iliyopita mbadala wa 'katuni', huwa wanatumia neno 'kiponzo'.
Nadhani 'kiponzo' au 'kibonzo' ni jitihada za kuongeza misamiati, badala ya 'kuhalalisha' matumizi ya 'katuni', neno ambalo lilikuwa linatumika toka enzi za utoto wetu.
a
a
Kibonzo
Kwa Kibonzo someni hapa
http://sw.wikipedia.org/wiki/Kibonzo
Nani anapenda kusahihsia kitu?